1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Rais Lula wa Brazil anafanya ziara nchini Marekani

10 Februari 2023

Rais wa Brazil Luiz Lula da Silva anafanya ziara nchini Marekani Ijumaa leo kwa mwaliko wa rais Joe Biden akilenga kuimarisha mahusiano yaliyofifia.

https://p.dw.com/p/4NJoL
Brasilien Präsident Lula da Silva Planalto Palace in Brasilia
Picha: Sergio Lima/AFP

Mahusiano kati ya mataifa hayo mawili yalififia wakati wa utawala wa rais Jair Bolsonaro.

Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva anafanya ziara nchini Marekani Ijumaa leo kwa mwaliko wa rais Joe Biden akilenga kuimarisha mahusiano yaliyofifia kati ya mataifa hayo mawili wakati wa utawala wa mtangulizi wake Jair Bolsonaro.

Akiwa mjini Washington Lula atakutana kwanza majira ya asubuhi na wanasiasa wa chama Democratic ikiwemo seneta Bernie Sanders kabla ya baadaye mchana kufanya mazungumzo na rais Biden katika ikulu ya White House.

Ziara hiyo itakajikita katika kuimarisha uungaji mkono wa Marekani kwa demokrasia ya Brazil, haki za binadamu  pamoja na masuala ya pamoja ya ulinzi wa mazingira.

Brazil inatafuta washirika wa kusaidia juhudi zake za kulinda mazingira hususani katika kuhifadhi msitu mkubwa wa Amazon unoachangia kwa kiasi kikubwa ufyonzaji wa gesi ya ukaa.