1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiBrazil

Rais Lula aongoza mamia kwa maelfu kumuaga Pele

3 Januari 2023

Zaidi ya watu laki mbili akiwemo Rais Luiz Inacio Lula da Silva wametoa heshima zao kwa nguli wa soka wa Brazil Pele, kwenye uwanja wa Vila Belmiro.

https://p.dw.com/p/4LhED
Brasilien Santos | Trauer nach Tod des Fußballspielers Pelé | Präsident Luiz Inacio Lula da Silva
Picha: Carla Carniel/REUTERS

Rais Lula ambaye aliapishwa siku ya Jumapili alisimama kando na jeneza la Pele, likiwa limepambwa kwa maua na bendera ya Brazil katika uwanja huo wa soka.

Watu mashuhuri akiwemo Rais wa shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA Gianni Infantino alikuwa ni miongoni mwa watu wa awali kutoa heshima zao za mwisho.

Msafara uliobeba jeneza la Pele unatazamiwa kupita katika mitaa ya Santos baadaye leo, ikiwa ni pamoja na kitongoji anachoishi mama yake mwenye umri wa miaka 100, na kisha kwenye makaburi maalum, ambapo atazikwa katika hafla ya faragha.