1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Kagame afanya uteuzi mpya wa mawaziri

5 Novemba 2019

Rais wa Rwanda Paul Kagame amemteua waziri mpya wa mambo ya nchi za kigeni katika mabadiliko ya baraza la mawaziri aliyoyafanya Jumatatu usiku.

https://p.dw.com/p/3SUCC
Ruanda - Afrika-CEO-Forum in Kigali
Picha: picture-alliance/C. Ndegeya

Mwanadiplomasia mkuu wa nchi hiyo, mwanasiasa mkongwe Vincent Biruta, atachukua nafasi ya Richard Sezibera ambaye hajaonekana hadharani kwa miezi kadhaa. Kutoonekana hadharani kwa Sezibera kumezusha uvumi kuwa huenda anaugua. Biruta amekuwa  waziri wa mazingira tangu Agosti 2017 lakini alishikilia nyadhifa nyingine ikiwemo rais wa Seneti kati ya mwaka wa 2003 hadi 2011. Pia ni kiongozi wa chama cha Social Democratic - SDP ambacho kipo katika muungano na chama tawala cha Rwandan Patriotic Front - RPF kinachoongozwa na Kagame. Mabadiliko mengine yaliyofanywa yalimhusisha Patrick Nyamvumba aliyeteuliwa kuwa waziri wa usalama wa ndani. Alikuwa  mkuu wa majeshi.