1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVietnam

Biden asifu enzi mpya ya uhusiano na Vietnam

11 Septemba 2023

Rais Joe Biden wa Marekani aliye ziarani nchini Vietnam amesema leo kuwa mahusiano baina ya mataifa hayo mawili yameingia "enzi mpya" kiasi miaka 50 tangu kumalizika kwa vita vya Vietnam.

https://p.dw.com/p/4WBkw
Rais Joe Biden amesifu hatua ya kuanza upya kwa mahusiano baina ya mataifa hayo mawili.
Rais Joe Biden akiwa na wakuu wa ngazi za juu wa Vietnam, wakati rais huyo alipofanya ziara nchini humoPicha: Luong Thai Linh/AP/picture alliance

Akizungumza kwenye kongamano la biashara mjini Hanoi kabla ya kuhitimisha ziara yake nchini humo, rais Joe Biden amesema Marekani na Vietnam zimetanua ushirikiano wao kwenye sekta muhimu, ikiwemo teknolojia mamboleo.

"Tunatanua ushirikiano wetu kwenye teknolojia muhimu, kama kuhifadhi pamoja data za mtandao, mawasiliano ya masafa na teknolojia ya akili bandia. Na pamoja tunawainua watu wetu ikiwemo kuzindua miradi mipya nchini Vietnam."

Biden aliwasili Vietnam jana kwa ziara ya siku moja ya kuimarisha mahusiano na taifa hilo la kusini mashariki mwa Asia ambalo lilishuhudia vita vya kutisha katikati mwa miaka 1950 hadi 1970.  Alikutana na Waziri Mkuu, Pham Minh Chinh na kiongozi wa chama cha kikomunisti cha Vietnam, Nguy·n Phú Trong.