1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden amwita Putin kuwa mhalifu wa kivita

17 Machi 2022

Wakatu hali ikiendelea kuwa mbaya nchini Ukraine, Rais Joe Biden wa Marekani amemwita rais wa Urusi Vladimir Putin kuwa ni mhalifu wa kivita.

https://p.dw.com/p/48bEr
USA Präsident Joe Biden Rede zur Lage der Nation
Picha: Saul Loeb/Getty Images

Msemaji wa Ikulu ya Urusi, Kreamlin Dmitry Peskov amesema kitendo cha rais wa Marekani Joe Biden kumwita Rais wa Urusi kuwa mhalifu wa kivita hakikubaliki na hakisameheki. Habari hizo ni kwa mjibu wa shirika la habari la taifa hilo TASS.

Rais Joe Biden wa Marekani amemwita rais wa Urusi Vladimir Putin kuwa ni mhalifu wa kivita, katika kipindi hiki ambacho matukio ya kikatili yakitajwa kuongezeka nchini Ukraine huku rais wa Ukraine akiliomba bunge la Marekani msaada zaidi.

Kauli hiyo inatazamwa kuwa kali zaidi kutoka Marekani tangu Urusi iivamie Ukraine. Wakati mataifa mengine yalitumia neno hilo lakini Marekani imekuwa ikijizuia.

Katika hotuba yake ya Jumatano Biden amesema vikosi vya Urusi vimeshambulia hosiptali na kuwachukua mateka madaktari. Hata hivyo ametoa ahadi zaidi kwa Ukraine katika kukabiliana kivita na Urusi. Amesema Marekani itatoa msaada wa nyongeza wa kijeshi wa kiasi cha dola milioni 800, na kufanya kiwango cha msaada kufikia jumla ya dola bilioni mbili tangu aingie madarakani mwaka mmoja uliopita.

Slovakia inatafakari kuipa Ukraine mfumo wa kujikinga na mashambulizi ya angani.

Ukraine Kiew | Belarussische Freiwillige erhalten Training
Mwanajeshi akiwa mazoezini mjini KyivPicha: Efrem Lukatsky/AP/picture alliance

Maafisa wa ulinzi wa Slovakia wanatarajiwa kujadili uwezekano wa kupeleka mfumo wa ulinzi wa zama za uliokuwa umoja wa Kisovieti aina ya S-300 wa ulinzi wa anga, pale Waziri wa Ulinzi wa Marekani atakapo wasili nchini humo Alhamis hii kwa mashauriano zaidi.

Mfumo huo ndio ule ambao Rais wa Ukraine Volodymir Zelensky aliutaja pale alipozungumza na wabunge wa Marekani kwa kusema utaweza kuifunga anga ya Ukraine dhidi ya mashambulizi ya anga ya Urusi na makombora yake.

Jengo la michezo linalodaiwa kuwa na mamia ya watu lashambuliwa na Urusi Mariupol.

Ndani nchini Ukraine, wizara ya mambo ya nje imesema vikosi vya Urusi vimelishambalia jengo la micherzo la mji wa mji wa Mariupol, ambalo inadaiwa mamia ya watu wamepatiwa hifadhi baada ya makazi yao kuharibiwa na mapigano. Shambulizi kutoka angali linaelezwa kulipasua katikati jengo hilo.

Ukraine-Konflikt - Charkiw
Jengo lililovurugwa vibaya mjini CharkiwPicha: Pavel Dorogoy/AP/dpa/picture alliance

Meya wa mji wa Kyiv Vitali Klitschko amesema makombora ya Urusi yameharibu maeneo kadhaa ya makazi ya watu na hasa katika kitongoji cha Podii, umbali wa kilometa 2.5 kutoka katika makao makuu ya serikali, ambayo pia yanajumuisha makazi ya rais, ofisi ya rais na ofisi nyingine muhimu.

Lakini taarifa hiyo haikuweza kufafanua juu ya athari zaidi zilizotokea kama kuna vifo au la. Wakazi wa Kyiv wamejificha katika makazi yao na maeneo maalumu baada ya kutolewa marufuku ya kutoka nje. Habari za mapema mjini humo zinasema jengo la ghorofa 12 liliwaka moto baada ya kushambuliwa na makombora ya Urusi.

Meya wa mji wa Melitapol alietekwa siku tano zilizopita Andriy Yermak apatikana.

Huko mjini Melitopol, Meya wa mji huo wa kusini/mashariki ameachiwa huru baada ya kutekwa na majeshi ya Urusisiku tano zilizopita. Andriy Yermak mkuu wa majeshi wa taifa hilo alitoa taarifa hizo pasipo ufafanuzi zaidi wa namna gani Fedorov aliachiwa huru.

Video ya usalama ya juma lililopita ilimuonesha Fedorov akitolewa nje ya jengo la jiji huku akiwa amezungukwa na askari wa Urusi.

Vyanzo AP/RTR