1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMauritania

Rais Ghazouani aongoza katika uchaguzi wa urais Mauritania

30 Juni 2024

Rais wa Mauritania Mohamed Ould Ghazouani anaongoza katika uchaguzi wa rais nchi humo.

https://p.dw.com/p/4hgnM
Rais wa Mauritania Mohamed Ould Ghazouani
Rais wa Mauritania Mohamed Ould GhazouaniPicha: Stringer/REUTERS

Matokeo ya awali ya tume ya uchaguzi yanaashiria kuwa kiongozi huyo anaongoza kwa asilimia 54.87 ya  kura zilizohesabiwa,  huku mpinzani wake wa karibu, mwanaharakati wa kupinga utumwa Biram Dah Abeid, akifuata kwa asilimia 22.86.

Kulingana na tovuti ya tume hiyo, takriban asilimia 50.32 za kura zimehesabiwa, sawa na vituo 2,211 kati ya vituo 4,503.

Ghazouani, mkuu wa zamani wa jeshi na mwenye umri wa miaka 67, anatarajiwa kushinda na ameahidi kuongeza uwekezaji katika taifa hilo la Afrika Magharibi lenye watu milioni 5.