1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Buhari kikaangoni

10 Mei 2021

Changamoto za kiusalama zinazoikabili Nigeria zimeibua hasira na wito wa kumtaka Rais Muhammadu Buhari aachie madaraka au aondolewe ofisini. Wachambuzi wanasema kuna hamu ya kumpindua Rais.

https://p.dw.com/p/3tCM6
Nigeria Kaduna | Polizeieinheit steht Wache in Unguwar Busa
Picha: Christina Aldehuela/AFP/Getty Images

Ripoti ya ujasusi iliyotolewa na makachero wa polisi imeonya kwamba wanasiasa wa zamani na wa sasa pamoja na viongozi wa dini walikuwa wanapanga kumwondoa madarakani Rais Buhari. Soma zaidiRais Buhari akabiliwa na shinikizo la ukosefu wa usalama 

Ripoti hiyo iliyochapishwa na Huduma ya Usalama wa Jimbo ilikuja siku chache tu baada ya jeshi kuahidi kutii katiba na kujikita chini ya utawala wa raia, na ikionya wanachama wake kujiepusha na siasa.

Wanigeria wanasema hali imekuwa mbaya chini ya utawala wa Buhari tangu alipoingia madarakani mnamo 2015, huku muhula wake wa pili na wa mwisho ukitarajiwa kumalizika mnamo 2023. Soma zaidi Zaidi ya wanajeshi 30 wauwawa na wanamgambo Nigeria

Wanafunzi kutekwa

Nigeria Demonstration gegen die Entführung von Schulmädchen
Picha: PIUS UTOMI EKPEI/AFP/Getty Images

Fatima Mohammed msichana mwenye umri wa miaka 23 akielezea madhila aliyopitia mikononi mwa watekaji nyara ambapo akikaa kwa siku 57.

"Nimepigwa na kuteswa, haswa wakati [majambazi] walipozungumza na wazazi wetu na kurudi bila habari njema. Wanatutesa kwa fimbo na bunduki zao." amesema Fatima.

Fatma ni miongoni mwa wanafunzi 27 waliotekwa nyara mwezi machi kutoka chuo cha misitu nchini Nigeria jimbo la Kaduna.

Yaliomkuta Fatima yanalingana na maisha ya wanawake na wanaume wengi wanaoishi Kaskazini mwa Nigeria waliowahi kutekwa na kudhulumiwa.

Kulingana na mwanaharakati wa kutetea haki za binaadam Dkt Auwal Aliyu, zaidi ya wanafunzi 800 wametekwa nyara shuleni wengi wao wakiwa ni wasichana.

"Watoto wanaogopa kwenda shule; wazazi hawana raha tena kuwapeleka watoto shule. Hiyo itakuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya elimu Kaskazini mwa Nigeria, na elimu ni uti wa mgongo wa kila kitu." amesema Dkt Auwal Aliyu. Soma zaidi Utekaji Nigeria wafikia kiwango cha mzozo

Nigeria Katsina | Präsident Muhammadu Buhari
Picha: Sunday Alamba/AP/picture alliance

Akizungumza kupitia njia ya simu mchambuzi wa maswala ya usalama Dkt Kabiru Adamu amesema, Kuzorota kwa usalama kote Nigeria kumezua hasira na hofu. Sasa uvumi umeenea kwamba mapinduzi ya kijeshi au mashtaka dhidi ya Rais Muhammadu Buhari yanakaribia.

Dkt Adamu ameongezea kuwa Ikiwa mapinduzi yatatokea, hayatatekelezwa na majenerali wanaohudumu kwa sababu wanafaidika na mfumo. Aidha mchambuzi huyo amesema upatanishi kati ya wanasiasa na maafisa wa jeshi wenye kinyongo ufanya uwezekano wa mapinduzi kuwa makubwa.