1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Ahmadinejad wa Iran akataa matakwa ya Umoja wa Mataifa

17 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CciY

Rais wa Iran, Mahmoud Ahmedinejad, kwa mara nyengine tena ameyakataa matwaka ya Umoja wa Mataifa yanayoitaka Iran ikomeshe mpango wake wa urutubishaji wa madini ya uranium.

Akizungumza katika televisheni ya taifa, rais Ahmadinejad amesema utawala wake mjini Tehran hautakubali shinikizo lolote la kuwekewa vikwazo vya kiuchumi wala harakati ya kijeshi dhidi yake. Nchi tano wanachama wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Ujerumani zinajadiliana uwezekano wa kuiwekea vikwazo zaidi Iran.

Rais Ahmadinejad amesema kuchapishwa kwa ripoti ya Marekani iliyosema Iran ilisitisha mpango wake wa nyuklia tangu mwaka wa 2003 ni kama tangazo la serikali ya mjini Washington kwamba imeshindwa katika mgogoro wake na serikali ya Tehran kuhusu mpango wa nyuklia.