1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raimondo na Le Keqiang watoa wito wa ushirikiano

29 Agosti 2023

Waziri wa biashara wa Marekani Gina Raimondo, amekutana Jumanne na waziri mkuu wa China Li Qiang na kutoa wito kwa China na Marekani zishirikiane katika kuyatatua masuala muhimu ya dunia.

https://p.dw.com/p/4Vi6J
Waziri wa biashara wa Marekani amemwambia waziri mkuu wa China  kwamba, Marekani inataka kushirikiana na China katika masuala muhimu ya dunia.
Waziri wa biashara wa Marekani amemwambia waziri mkuu wa China  kwamba, Marekani inataka kushirikiana na China katika masuala muhimu ya dunia.Picha: Andy Wong/REUTERS

Ziara ya waziri Raimondo nchini China inafuatia nyingine za hivi karibuni zilizofanywa na wajumbe wa Marekani wa ngazi za juu kwa lengo la kupunguza mivutano na China, nchi inayoshika nafasi ya pili duniani katika nguvu za kiuchumi.

Waziri wa biashara wa Marekani amemwambia waziri mkuu wa China  kwamba, Marekani inataka kushirikiana na China katika masuala muhimu ya dunia, ikiwa pamoja na mabadiliko ya tabia nchi, teknolojia ya akili bandia na katika juhudi za kupambana na uraibu wa madawa makali yanayotumika kutuliza maumivu.

Waziri huyo wa Marekani pia leo hii alikutana na viongozi wengine wa China ambapo alisisitiza umuhimu wa kuweka wazi njia za mawasiliano baina ya mataifa yao makubwa.