1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wa Uganda waishitaki kampuni ya mafuta ya Total

27 Juni 2023

Raia 26 wa Uganda wamefungua mashatka dhidi ya kampuni kubwa ya kuchimba mafuta ya Ufaransa ya Total wakitaka kulipwa fidia kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu kwenye miradi mikubwa ya kampuni hiyo.

https://p.dw.com/p/4T8Ip
Frankreich Protest gegen Rentenreform Bildergalerie
Picha: LOIC VENANCE/AFP/Getty Images

Wakiwa wameungana na raia wengine wa tano na makundi ya msaada ya Ufaransa, watu kutoka jamii zilizoathirika zimesema kampuni ya Total imesababisha "madhara makubwa" hususani kwa haki zao za kupata ardhi na chakula. 

Wameitaka mahakama ya mjini Paris kutambua dhima inayopaswa kubebwa na kampuni hiyo na iamuru ilipe fidia watu wote walioathirika na shughuli zao.

Soma zaidi: Mahakama ya Ufaransa yapuulizia mbali kesi dhidi ya kampuni ya TotalEnergies

Miradi inayolalamikiwa ni ule wa utafutaji mafuta kwenye visima 419 huko Tilenga na ujenzi wa bomba kubwa la kusafirisha nishati hiyo kutoka Uganda hadi pwani ya Bahari ya Hindi nchini Tanzania. 

Wakati kesi hiyo ikifunguliwa, waandamanaji kadhaa walizimavia hii leo ofisi za kampuni ya Total nchini Uingereza na kupuliza rangi kwenye lango na eneo la mapumziko ya wageni kuonesha upinzani kwa ujenzi wa bomba la mafuta la Afrika Mashariki.

Polisi imesema watu 27 wamekamatwa huku kampuni ya Total ikilaani maandamano hayo ya vurugu.