1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wa Misri washiriki uchaguzi mkuu

10 Desemba 2023

Raia wa Misri wanashiriki uchaguzi wa urais wakati zoezi zima likigubikwa na vita vya Gaza na mgogoro mkubwa wa kiuchumi huku rais wa sasa akitarajiwa kuchukua ushindi

https://p.dw.com/p/4ZzGl
Misri I Uchaguzi
Baadhi ya raia wa Misri wakishiriki uchaguzi mkuu mjini CairoPicha: Amr Nabil/AP/picture alliance

Uchaguzi huo unafanyika kwa siku tatu hadi siku ya Jumanne, na rais anayetetea kiti chake Abdel-Fattah al-Sissi, anatarajiwa kushinda muhula wa tatu madarakani. 

Al-Sissi, aliyeiongoza Misri tangu mwaka 2014, alipiga kura katika kituo cha kupigia kura cha Heliopolis, Mashariki mwa mji mkuu Cairo, na baada ya hapo hakutoa tamko lolote juu ya zoezi hilo. 

Licha ya matatizo ya kupanda kwa gharama ya maisha, al-Sissi amepata uungwaji mkono kufuatia Wamisri wengi kukubaliana na onyo alilolitoa dhidi ya hofu ya watu wa Gaza waliopoteza makaazi yao kuingia nchini humo. 

Misri yawapokea majeruhi kutoka Ukanda wa Gaza

Tangu kuanza kwa vita kati ya Israel na Hamas al Sissi ametahadharisha kuwa kuwapeleka Wapalestina nchini mwake kutaibadilisha rasi hiyo ya Sinai kuwa ngome ya kuanzisha mashambulizi dhidi ya Israel. 

Raia milioni 67 wa Misri wanatarajiwa kushiriki uchaguzi huo, ulio na wagombea wengine watatu.