1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wa Algeria wanapiga kura leo katika uchaguzi wa rais

Sylvia Mwehozi
7 Septemba 2024

Raia wa Algeria wanapiga kura leo katika uchaguzi wa rais unaotarajiwa kumwongezea muhula mwingine wa miaka mitano madarakani rais Abdelmadjid Tebboune.

https://p.dw.com/p/4kNk3
Abdelmadjid Tebboune / Rais wa Algeria
Rais Abdelmadjid Tebboune wa Algeria.Picha: Photoshot/picture alliance

Raia wa Algeria wanapiga kura leo katika uchaguzi wa rais unaotarajiwa kumwongezea muhula mwingine wa miaka mitano madarakani rais Abdelmadjid Tebboune.

Rais Tebboune, mwenye umri wa miaka 78, anapewa nafasi kubwa ya kumshinda mgombea Muislamu mwenye msimamo wa wastani Abdelaali Hassani na mgombea wa kisoshalisti Youcef Aouchiche katika kinyang'anyiro cha kuongoza nchi hiyo ya Afrika Kaskazini.

Changamoto kubwa inayomkabili kiongozi huyo ni kuongeza idadi ya wapiga kura watakaojitokeza, baada ya kushinda mwaka 2019 kwa asilimia 58 ya kura. Idadi ndogo ya wapiga kura waliojitokeza 2019 ilifuatia maandamano ya kuunga mkono demokrasia ya Hirak, ambayo yalimuondoa rais wa zamani Abdelaziz Bouteflika kabla ya kukomeshwa na polisi. Mamia ya waandamanaji walitiwa nguvuni.

Zaidi ya Waalgeria 800,000 wanaoishi nje ya nchi tayari walianza kupiga kura.