1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Raia kiasi 13 wauliwa Mali na wapiganaji wa jihadi

29 Juni 2023

Raia wapatao 13 wameuliwa na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa jihad kaskazini mwa Mali. Maafisa wamesema watu wengine kadhaa walijeruhiwa.

https://p.dw.com/p/4TDKg
Mali Unruhen Soldaten
Picha: Sebastien Rieussec/Hans Lucas/IMAGO

Hayo ni kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa jana Jumatano na maafisa waliochaguliwa kwa njia ya kura kuwawakilisha wananchi walioomba wasitambulishwe majina yao.

Afisa wa eneo hilo alisema watu wengine kadhaa walijeruhiwa katika uvamizi huo na mamia ya wengine wakalazimika kukimbia kutoka vijijini mwao eneo la Gabero katika eneo pana la Gao.

Afisa huyo aidha alisema jeshi la Mali halikuwepo katika eneo hilo. Mashariki mwa Gabero, Gao na Menaka ni maeneo ambayo yamekuwa uwanja wa operesheni kubwa dhidi ya kundi linalojiita Dola la Kiislamu ukanda wa Sahara, ISGS tangu mwanzoni mwa mwaka uliopita.