1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia 10 wa DRC wauawa katika mapigano ya mjini Khartoum

6 Juni 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Christophe Lutundula amesema raia wa nchi hiyo wapatao 10 wamekufa kufuatia mashambulizi ya Siku ya Jumapili, yaliyoendeshwa na Jeshi la Sudan.

https://p.dw.com/p/4SEu7
Sudan | Khartoum
Moshi mkubwa ukifuka mjini KhartoumPicha: Mohamed Nureldin Abdallah/REUTERS

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Christophe Lutundula amesema raia wa nchi hiyo wapatao 10 wamekufa kufuatia mashambulizi ya Siku ya Jumapili, yaliyoendeshwa na Jeshi la Sudan katika kampasi ya chuo kikuu cha Kimataifa cha Afrika mjini Khartoum. Lutundula amesema alifanya mazungumzo hapo jana na maafisa wa ubalozi wa Sudan mjini Kinshasa na kuwasilisha "ujumbe wa kero na huzuni" na kusisitiza kuwa Kongo imeomba maelezo zaidi juu ya tukio hilo pamoja na hatua kutoka kwa serikali ya Sudan ili kuruhusu kusafirishwa kwa miili hiyo. Tangu kuanza kwa mzozo wa Sudan Aprili15, mji mkuu wa Khartoum umekuwa kitovu cha uhasama. Raia wa Sudan na wale wa kigeni wamekuwa wakinaswa katika mapigano hayo. Mzozo huo kati ya majenerali wawili hasimu tayari umesababisha vifo vya watu 1,800.