1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RABAT:Afrika na Ulaya zakubaliana kupambana na wahamiaji wa kinyume cha sheria

12 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG8M

Wajumbe wa serikali kutoka nchi zaidi ya 50 za Ulaya na Afrika wameafikiana juu ya kuzindua zama mpya za ushirikiano katika kupambana na uhamiaji wa kinyume cha sheria.

Wajumbe hao walikubaliana kwenye mkutano wao wa mjini Rabat nchini Morocco juu ya mpango wa kuunga mkono uhamiaji halali, kutoa msaada wa fedha kwa nchi za Afrika na kupambana na wahalifu wanaosafirisha wahamiaji kinyume cha sheria.

Makubaliano ya nchi za Ulaya na Afrika pia yanahusu pendekezo juu ya kuratibisha udhibiti wa mipaka,bandari na njia zinazotumiwa na wahamiaji pamoja na kujenga kituo cha kufuatilia nyendo za wahamiaji hao,sambamba na kuwatanabahisha juu ya hatari zinazoweza kuwakabili.