1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RABAT : Wito kwa mkutano wa Umoja wa Ulaya na Afrika kujadili wahamiaji

12 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CESt

Morocco na Uhispania hapo jana zimeitisha mkutano wa Umoja wa Ulaya na Afrika kwa kuzijumuisha pamoja nchi zilizoathirika na uhamiaji.

Akiwa katika ziara fupi mjini Rabat kufuatia majaribio kadhaa ya wahamiaji wa Afrika Magharibi kuvamia maeneo ya ardhi ya Uhispania yalioko nchini Morroco katika wiki za hivi karibuni waziri wa mambo ya nje wa Uhispania Miguel Angel Moratinos amesema mkutano huo utazijumuisha pamoja nchi zinazotowa wahamiaji hao wasio halali, nchi wanakopitia kwa muda na nchi wanazokusudia kwenda kuloweya.

Umoja wa Afrika pia umeunga mkono wito huo wa kuwepo kwa mazungumzo kati ya Umoja wa Ulaya na Afrika.

Msemaji wa Umoja wa Afrika Adam Thiam amesema kile kinachotokea nchini Uhispania na Morocco wakati huu huku wahamiaji wakifa na kutupwa baharini kunadokeza kwamba ni mazungumzo tu kati ya Umoja wa Ulaya na Afrika ndio yanayoweza kutowa ufumbuzi wa tatizo hilo.

Amesema huo ni ufumbuzi wa pekee kwa kioja hicho cha aibu.