1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rabat. Wahamiaji haramu kurejeshwa kutoka Hispania.

7 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEUK

Vyombo vya habari vya Morocco vimesema kuwa watu 6 kutoka mataifa ya Afrika wameuwawa katika mapambano na wanajeshi wa nchi hiyo ambao walikuwa wakilinda uzio wa waya unaozunguka eneo moja la Hispania la Melilla.

Hii ni moja kati ya majaribio kadha yanayofanywa na wale wanaotaka kuwa wahamiaji kinyume na sheria wanaojaribu kuingia katika eneo hilo la Melilla pamoja na eneo jingine la Hispania katika pwani ya kaskazini ya Morocco, ya Ceuta.

Hispania wakati huo huo imetangaza kuwa inawarejesha Waafrika 70 nchini Morocco , kama sehemu ya sera yake mpya ya kuwarejesha watu ambao wanaingia katika maeneo ya Melilla na Ceuta kinyume na sheria.

Waziri mkuu msaidizi wa Hispania Maria Teresa Fernandez de la Vega ametoa taarifa hiyo wakati akiwa katika ziara ya Ceuta, ambako watu watano wamekufa wiki iliyopita wakijaribu kuingia katika eneo hilo.