1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RABAT: Viongozi wajadiliana tatizo la uhamiaji

11 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG8e

Mawaziri kutoka nchi za Umoja wa Ulaya na bara Afrika wanaendelea na mkutano wao wa siku mbili katika mji mkuu wa Morocco,Rabat.Mawaziri hao wanajaribu kutafuta njia za kukabiliana na uhamiaji wa kinyume cha sheria.Hii ni mara ya kwanza kwa mawaziri wa Ulaya na wa nchi zinazotumiwa kusafiria,kukutana pamoja kulijadili suala hilo.Umoja wa Ulaya unataka msaada kutafuta njia za kuimarisha ulinzi mipakani na kukomesha biashara ya kusafirisha binadamu.Wajumbe mkutanoni wanajaribu pia kutafuta njia ya kukabiliana na matatizo yanyosababisha uhamiaji huo kama vile umasikini,machafuko na ukosefu wa maendeleo katika nchi nyingi za Kiafrika.