1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pyongyang yaishutumu IAEA kuhusu maji ya Fukushima

Sylvia Mwehozi
9 Julai 2023

Korea Kaskazini imelishutumu Shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti nishati ya nyuklia IAEA, kwa kuidhinisha mpango wa Japan wa kutiririsha maji baharini kutoka kinu cha nyuklia cha Fukushima.

https://p.dw.com/p/4TdPp
IAEA Grossi akitembelea Fukushima
Mkuu wa IAEA Rafael Mariano Grossi, alipotembelea kinu cha nyuklia cha Fukushima.Picha: The Associated Press/REUTERS

Korea Kaskazini imelishutumu Shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti nishati ya nyuklia IAEA, kwa kuidhinisha mpango wa Japan wa kutiririsha maji baharini kutoka kinu cha nyuklia cha Fukushima. Mpango huo umeibua wasiwasi katika nchi jirani, hali iliyosababisha China kupiga marufuku baadhi ya vyakula kutoka nje na kuzuka kwa maandamano nchini Korea Kusini

Afisa mmoja kutoka wizara ya ulinzi wa mazingira ya Korea Kasakazini, amenukuliwa na shirika la habari la KCNA akisema kwamba utiririshaji huo wa maji yaliyosafishwa utakuwa na athari mbaya kwa maisha ya binadamu, usalama na mazingira ya kiikolojia.

Soma pia: Mkuu wa IAEA azuru kinu cha Fukushima nchini Japan

Pyongyang imetoa angalizo hilo wakati mkuu wa shirika la IAEA  Rafael Grossi akikamilisha ziara yake ya siku tatu nchini Korea Kusini, alikokutana na wabunge wa upinzani ambao wamekosoa vikali mpango huo.