1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PYONGYANG Korea Kazkazini yakataa mazungumzo kuhusu mpango wake wa nuklia

8 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF5h

Korea Kazkazini imesema haitashiriki katika mazungumzo kuhusu mpango wake wa nuklia mpaka Marekani iyakubali masharti yake.

Haya yamesemwa baada ya mjumbe wa Uchina katika umoja wa mataifa kutangaza kwamba Korea Kazkazini huenda ikaanza tena mazungumzo juu ya mpango wake wa nuklia na mataifa sita katika kipindi cha majuma machache yajayo mjini Beijing. Wang Guangya, ambaye nchi yake ni mshiriki wa karibu wa Korea Kazkazini, amesema njia ya mazungumzo ndiyo njia muhimu ya pekee ya kuutanzua mzozo huo.

Mkutano wa mwisho uliozishirikisha Korea Kazkazini, Korea Kusini, Marekani, Russia, Uchina na Japan, ulifanyika yapata mwaka mmoja uliopita. Mwezi Februari mwaka huu Korea Kazkzini ilitangaza kwamba ina miliki silaha za kinuklia.