PYONGYANG: Fedha za Korea kurejeshwa kutoka Macau
14 Juni 2007Matangazo
Fedha za Korea Kaskazini zinazozuiwa kwenye benki moja ya Macau zitaanza kurejeshwa leo.
Shirika la habari la Japan limesema hatua hiyo huenda ikasaidia kutanzua mzozo unaoendelea wa mradi wa silaha za kinyuklia wa Korea Kaskazini.
Serikali ya Korea Kaskazini imelikataa pendekezo ililowekewa la kufunga kituo cha Yongbyon cha nishati ya kinyuklia kuanzia mwezi Februari mwakani hadi pale itakaporejeshewa fedha zake zilizoko Macau.
Fedha hizo zilizuiwa wakati Marekani ilipoishutumu benki ya Banco Delta Asia kwa kufanya biashara haramu na serikali ya Korea Kaskazini.