1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putina asema mapigano ya Zaporizhzhia ni makali

27 Julai 2023

Rais Vladimir Putin wa Urusi amesema leo mapigano yamezidi mno katika eneo la Zaporizhzhia kusini mashariki mwa Ukraine.

https://p.dw.com/p/4UU4V
Ukraine, Saporischschja | Soldatinnen trainieren für den Einsatz an der Front
Picha: Ercin Erturk/AA/picture alliance

Putin ambaye yuko mjini Saint Petersburg, amewapongeza wanajeshi wake kwa kile alichosema ni kuzuia mashambulizi ya Ukraine na kudai kwamba wamelitia hasara kubwa jeshi la Ukraine.

Madai ya Putin lakini hayajaweza kuthibitishwa na vyanzo huru.

Kulingana na maafisa wa nchi za Magharibi na Ukraine na hata wachambuzi, Ukraine imeanzisha mchakato wa kuyatimua majeshi ya Urusi kutoka kusini mashariki mwa nchi hiyo, kama sehemu ya mashambulizi yake ya wiki nzima ya kulipiza kisasi, ambapo wamepeleka maelfu ya majeshi katika eneo la mapambano.

Kumekuwa na mapigano makali katika wiki za hivi karibuni katika maeneo kadhaa huko Zaporizhzhia ambako majeshi ya Urusi yalivamia miezi 27 iliyopita.