1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin asema mizozo inaimarisha uhusiano wa Urusi na China

Sylvia Mwehozi
19 Oktoba 2023

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema migogoro inayoendelea ulimwenguni imezidi kuimarisha mahusiano ya nchi yake na China alipokutana na Rais Xi Jinping.

https://p.dw.com/p/4XjJe
China I Putin na Xi
Rais wa Urusi Vladimir Putin na rais wa China Xi JinpingPicha: Sergei Guneyev/Pool/picture alliance

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema migogoro inayoendelea ulimwenguni imezidi kuimarisha mahusiano ya nchi yake na China. Putin ametoa kauli hiyo mara baada ya kufanya mazungumzo na rais wa China Xi Jinpingkatika ziara yake ya kwanza kwenye taifa hilo lenye uchumi mkubwa duniani, tangu uvamizi wake nchini Ukraine.

Viongozi hao wawili walikutana mjini Beijing pembezoni mwa Kongamano la China linalohusu mradi mkubwa wa miundombinu ya barabara na Reli. Mazungumzo ya viongozi hao yaligubikwa na mzozo wa Mashariki ya Kati, huku rais Xi akisema kwamba anatumai Urusi na China zinaweza kufanya kazi pamoja katika kulinda haki za kimataifa.

Kongamano kuhusu mradi wa China wa Miundombinu ya barabara na reli katika nchi zinazoendelea, umehudhuriwa na wajumbe kutoka zaidi ya nchi 130 wakiwemo viongozi wa juu wa serikali.