1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Putin awasili Astana kushiriki mkutano wa Shanghai

Sylvia Mwehozi
3 Julai 2024

Rais wa Urusi Vladimir Putin amewasili katika mji mkuu wa Kazakhstan wa Astana leo Jumatano kushiriki mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai SCO.

https://p.dw.com/p/4hnpL
Vietnam | Wladimir Putin zu Staatsbesuch in Vietnam eingetroffen
Rais wa Urusi Vladimir Putin Picha: Minh Hoang/AP Photo/picture alliance

Putin anatazamiwa kukutana na rais wa China Xi Jinping na Tayyip Erdogan wa Uturuki.

Mara ya mwisho, Putin kukutana na Rais Xi ilikuwa mwezi Mei, wakati  alipoitembelea China katika ziara yake ya kwanza ya nje ya nchi baada ya kuapishwa kwa muhula wa tano kama rais wa Urusi.

Soma pia:Putin kusaini mikataba ya ushirikiano wakati wa ziara mjini Pyongyang 

Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai SCO ni jukwaa la kimataifa la kisiasa, kiuchumi, na kiusalama lililoanzishwa na China na Urusi mwaka 2001. Linajumuisha nchi wanachama ambao ni India, Iran, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Pakistan, Tajikistan na Uzbekistan.

Uturuki, ambayo si mwanachama wa jumuiya hiyo, mara nyingi imekuwa ikishiriki katika mikutano yake kama mbia wa mazungumzo.