1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMongolia

Putin atoa mwaliko kwa Mongolia kuhudhuria mkutano wa BRICS

3 Septemba 2024

Rais wa Urusi ametoa mwaliko kwa rais wa Mongolia Ukhnaagiin Khürelsükh wa kuhudhuria mkutano wa mataifa yanayoinukia kiuchumi, BRICS utakaofanyika kwenye mji wa Urusi wa Kazan mwishoni mwa mwezi wa Oktoba.

https://p.dw.com/p/4kEMf
Putin besuchtThubten Shedrub Ling
Rais wa Urusi Vladimir Putin atembelea "Thubten Shedrub Ling", nyumba ya watawa wa Kibudha mjini Kyzyl Urusi. Picha: KRISTINA KORMILITSYNA/AFP

Rais Vladimir Putin anayefanya ziara nchini Mongolia amesema anadhamiria hasa kuzungumzia juu ya ushirikiano wa kiuchumi na Mongolia.

Ziara ya Putin nchini Mongolia inazingatiwa kuwa ya utata kwa sababu Mongolia inaitambua mahakama ya kimataifa iliyotoa waranti wa kuwezesha kukamatwa kwa kiongozi huyo wa Urusi.

Soma pia: Putin asema uvamizi wa Ukraine Kursk haujawa na athari 

Hata hivyo hakuna dalili kwamba nchi hiyo mwenyeji itatekeleza wito wa kumkamata rais huyo wa Urusi kwa madai ya uhalifu wa kivita kutokana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Mongolia inayopakana na Urusi inamtegemea sana jirani yake huyo kwa mafuta na umeme.