1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Putin ataja shambulizi mjini Belgord kuwa 'tukio la kigaidi'

1 Januari 2024

Rais Vladimir Putin wa Urusi amesema kuwa mfululizo wa mashambulizi ya makombora ya Ukraine yaliyosababisha vifo vya takriban watu 20 na kujeruhiwa kwa wengine 111 katika mji wa Belgorod yalikuwa ''kitendo cha ugaidi''

https://p.dw.com/p/4am7O
Rais wa Urusi Vladimir Putin akilihutubia taifa mkesha wa mwaka mpya Mnamo Desemba 31,2023
Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Adrien Fillon/Zumapress/picture alliance

Akizungumza wakati wa mkutano na wanajeshi wake katika hospitali moja ya kijeshi mjini Moscow, Putin amesema lazima hatua ichukuliwe kutokana na mashambulizi hayo yaliyofanyika wakati wa Urusi ikiimarisha mashambulizi ya anga dhidi ya miji ya Kyiv na Kharkiv.

Putin amesema kuwa wanajeshi wake wataendelea kulenga ''shabaha muhimu za kijeshi nchini Ukraine." Hata hivyo, Urusi imekanusha shutuma za mataifa ya Magharibi na Ukraine kwamba inalenga miundombinu ya kiraia.

Soma pia:Urusi yadai kuzima mashambulizi ya Ukraine katika ardhi yake

Katika mazungumzo hayo yaliyogusia masuala mbali mbali, Putin amesema kuwa mkondo wa vita nchini Ukraine unageuka kwa manufaa yaUrusi na kwamba nchi hiyo inatumai kumaliza vita hivyo lakini kwa mujibu wa matakwa  yake.