1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin asifu mahusiano kati ya Urusi na Kazakhastan

9 Novemba 2023

Putin ameitembelea Kazakhastan leo ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kuimarisha mahusiano na taifa hilo la Asia ya Kati lililokuwa sehemu ya Muungano wa Kisovieti na ambalo ni mshirika muhimu wa kiuchumi wa Moscow.

https://p.dw.com/p/4Yctt
Rais wa Urusi Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Gavriil Grigorov/Sputnik/REUTERS

Akizungumza mwanzoni mwa mkutano wake na rais Kassym-Jomart Tokayev wa Kazakhastan, rais Putin ameyasifu mahusiano kati ya nchi hizo mbili na kusema wanalenga kuyaimarisha zaidi na kuyafanya kuwa ya kimkakati.

Ziara yake nchini humo inafuatia ile aliyoifanya mwezi uliopita nchini Kyrgyzstan kwa mkutano wa kilele wa mataifa yaliyounda Muungano wa Kisovieti na nyingine aliyoifanya hivi karibuni nchini China.

Kazakhastan taifa lenye utajiri mkubwa wa mafuta pamoja na matafa mengine ya Asia ya Kati yameendeleza mahusiano yao na Urusi licha ya shinikizo kutoka mataifa ya magharibi yanayoilamu Moscow kutokana na vita nchini Ukraine.