1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Putin asema Urusi iko tayari kwa makubaliano na Ukraine

9 Desemba 2022

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema huenda katika siku zijazo nchi yake ingeweza kufikia makubaliano kuhusu Ukraine, lakini alihisi kusalitiwa kutokana na kuvunjika makubaliano ya Minsk.

https://p.dw.com/p/4Kjqs
Russlands Präsident Wladimir Putin
Picha: Mikhail Metzel, Sputnik, Kremlin Pool Photo via AP/picture alliance

Rais Putin amesema Ujerumani na Ufaransa ambazo zilisimamia makubaliano ya usitishaji mapigano katika mji mkuu wa Belarus, Minsk, kati ya Ukraine na waasi wanaoungwa mkono na Urusi mashariki mwa Ukraine mnamo mwaka 2014 na 2015, ziliisaliti Urusi na sasa zimekuwa zikiipatia Ukraine silaha.

Rais Putin amesema suala si kufikia makubaliano bali kuwepo dhamana.

Hata hivyo, Putin ametahadharisha leo kwamba nchi yoyote itakayothubutu kuishambulia Urusi kwa silaha za nyuklia, basi nchi hiyo itafutwa katika ramani ya dunia.