1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin: Urusi iko tayari kwa mkataba wa kusafirisha nafaka

2 Agosti 2023

Rais wa Urusi Vladimir Putin, amemwambia mwenzake wa Uturuki Recip Tayyip Erdogan kuwa Moscow iko tayari kurudi kwenye mpango wa usafirishaji wa nafaka kupitia Bahari Nyeusi.

https://p.dw.com/p/4UhEN
Russland St. Petersburg | Marineparade
Picha: Alexander Kazakov/SNA/IMAGO

Lakini kwa mashartiya mataifa ya Magharibi kutimiza wajibu wake juu ya nafaka za Urusi. Katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Erdogan, Putin ameorodhesha sababu za Urusi kujiondoa kwenye mpango huo wa usafirishaji wa nafaka. Mpango huo uliruhusu usafirishaji salama wa nafaka za Ukraine kupitia Bahari Nyeusi.Urusi imeeleza kuwa mataifa ya Magharibi hayajafanya lolote kuwezesha usafirishaji wa nafaka na mbolea za Urusi, kama ilivyoainishwa kwenye makubaliano yaliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa na Uturuki mwezi Julai mwaka jana.Kwa upande wake, Rais wa Uturuki amemtolea mwito Putin kutozidisha mzozo kati ya Urusi na Ukraine baada ya Moscow kushambulia miundombinu ya bandari katika mkoa wa Odesa usiku wa kuamkia leo.