1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin anatabasamu licha ya shinikizo

10 Desemba 2019

Baada ya mkutano wa Paris kati ya Ukraine na Urusi ambapo wamekubaliana kusitisha mapigano kufikia mwishoni mwa mwaka huu, rais wa Ukraine anafikiri kwamba matokeo ni sare. Hapo ndipo anapokosea.

https://p.dw.com/p/3UWRO
Ukraine-Gipfel in Paris Zelensky Putin
Picha: Imago Images/ITAR-TASS

Katika uchambuzi wake mwandishi wa DW Bernd Riegert anaandika, majadiliano bila shaka yalikuwa rahisi sana kwa Putin kwasababu mwenzake, rais wa Ukraine, anajifanya kupendelea umoja ila kwa shingo upande. Rais Emmanuel Macron amemfuata rais Putin na kuzungumza naye kuhusu ushirikiano mpya ambao Urusi inastahili kuwa sehemu. Katika jambo hili Macron peke yake ndiye anayeonekana kuweka juhudi, ila Kansela Angela Merkel anaonekana kuwa mkimya, anaanza majadiliano haya kwa mguu mbaya.

Katika mkutano wa Jumuiya ya kujihami ya NATO wiki iliyopita, nchi za jumuiya hiyo zilizo mashariki mwa Ulaya ziliionya kuhusu Urusi, kwani Ufaransa inataka kuifanya Urusi ikubalike tena kijamii.

Mzozo wa Crimea haukujadiliwa rasmi Paris

Ufahamu kwamba Macron na Merkel wanamuwekea shinikizo Rais Zelensky asiwe na misimamo mikali na angalau afikie makubaliano. Hakuna kinachowezekana bila Urusi ingawa kuna ugumu wake Urusi inapokuwa sehemu ya jambo fulani. Kutokana na hali hii, Putin anaweza kuketi na kusubiri tu. Bila shaka anataka aondolewe vikwazo na Umoja wa Ulaya ila hilo si jambo linaloweza kumfanya aachie azma yake ya kutaka kulitawala eneo la Ukraine mashariki au hata Crimea.

Paris Ukraine-Gipfel Merkel Putin
Putin akijadiliana na Kansela Merkel na Rais MacronPicha: Reuters/C. Platiau

Isitoshe mzozo katika eneo hilo lililovamiwa hata haukujadiliwa rasmi Paris. Mzozo huo pia unafanya vigumu kwa Ukraine kutaka kuwa mwanachama wa Muungano wa Ulaya na NATO kwa kuwa miungano hiyo haikubali nchi zenye mizozo inayoendelea.

Nchi za Magharibi pamoja na Ukraine zinamhitaji Putin mno kiasi cha kwamba wanajadiliana naye ingawa wanamshuku kwamba ndiye aliyepanga kudunguliwa kwa ndege ya MH17 katika anga ya Ukraine, wanamshuku pia kuwa ndiye aliyehusika na shambulizi la sumu dhidi ya jasusi wa Urusi Sergei Skripal na mwanawe huko Uingereza na sasa wanahisi pia kwamba ndiye aliyehusika kupanga mauaji ya raia wa Georgia mjini Berlin.

Putin ni thibitisho la kiongozi mwenye nguvu

Kwa mtazamo wa Ujerumani na Ufaransa ni vigumu mno kupata makubaliano kuhusiana na chochote kutoka kwa Putin hasa ikizingatiwa kuwa uhusiano wao na mwanachama mkuu wa NATO, Marekani una shaka shaka. Rais Donald Trump kwasababu zisizojulikana anaamini kuwa Vladimir Putin ni mtu mzuri.

Frankreich Normandie | Gipfeltreffen: Vladimir Putin, Angela Merkel, Emmanuel Macron und Wolodymyr Selenskyj
Viongozi wa Ukraine, Ufaransa, Urusi na Ujerumani katika mkutano wa kilele ParisPicha: Getty Images/AFP/I. Langsdon

Iwapo bado Putin hajaonekana kama thibitisho la nguvu, ukiangalia mitaa ya Paris leo hii utalifahamu hilo kwani kuna maandamano ya hasira dhidi ya Emmanuel Macron. Na Angela Merkel naye? Kansela huyo wa Ujerumani aliyekuwa na mchango mkubwa katika mazungumzo ya Normandy mwaka 2014, amesikika kwa mbali tu huko Paris na muungano wake wa serikali nyumbani, unapitia wakati mgumu.

Kwa hiyo Putin ambaye ni mjanja mno, atajiuliza, kwanini niwakubalie matakwa yao sasa?