1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfrika Kusini

Putin ampongeza Ramaphosa kwa kuchaguliwa tena kuwa rais

18 Juni 2024

Rais wa Urusi Vladimir Putin amempongeza Cyril Ramaphosa kwa kuchaguliwa tena kama Rais wa Afrika Kusini na kuashiria kuwepo kwa uhusiano mzuri kati ya nchi hizo mbili.

https://p.dw.com/p/4hAzh
Russland | PK Wladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir Putin akizungumza na wanahabari katika kongamano la Urusi na Afrika katika Ikulu ya Constantine.Picha: Sergei Bobylev/TASS/dpa/picture alliance

Taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya ikulu ya Kremlin imeelezea matumaini ya kuimarika kwa ushirikiano kati ya Urusi na Afrika Kusini katika sekta mbalimbali.

Ramaphosa alichaguliwa tena na bunge siku ya Ijumaa kuwa Rais wa taifa hilo, japo hatua ya chama chake ANC kushindwa kupata wingi wa viti bungeni katika uchaguzi wa mwezi uliopita.

Soma pia:  ANC, DA wakubaliana kuunda serikali Afrika Kusini

Hiyo ikiwa kwa mara ya kwanza katika muda wa miaka 30 na kulazimisha kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa.

Uhusiano wa muda mrefu wa Urusi na Afrika Kusini - kama ilivyo kwa baadhi ya mataifa ya Afrika - ulianza nyakati za utawala wa muungano wa Kisovieti ambapo Urusi iliunga mkono harakati za mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi zilizoongozwa na ANC.