1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Putin aitolea Kyrgystan mwito wa kuimarisha uhusiano

12 Oktoba 2023

Rais Vladimir Putin wa Urusi ataka uhusiano wa kijeshi kati yao na Kyrgyzstan kuimarishwa

https://p.dw.com/p/4XT2m
Vladimir Putin, rais wa urusi.
Vladimir Putin, rais wa urusi.Picha: Pavel Bednyakov/REUTERS

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema ametoa mwito wa kuimarisha uhusiano wa kijeshi na Kyrgyzstan, katika ziara yake nchini humo, ambayo ni ya kwanza ya nje tangu Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC ilipotoa waranti wa kukamatwa kwake.

Picha za televisheni zimemuonyesha Putin akisalimia na rais Sadyr Japarov wa Kyrgyzstan, tayari kuhudhuria mkutano wa kilele wa kundi lililoundwa baada ya kuanguka kwa Umoja wa Kisovieti, CIS.

Putin amemwambia Jarapov kwamba anatarajia ushirikiano wa kijeshi na ufundi wa jeshini kati ya Urusi na Kyrgyzstan utaendelea kuimarika na kupanuliwa.

Hata hivyo ziara hiyo inafanyika katikati ya mgawanyiko miongoni mwa washirika wa Urusi. Kiongozi wa Armenia Nikol Pashinyan hatahudhudhuria mkutano huo ambao Putin anashiriki, akiituhumu Moscow kwa kushindwa kuingilia wakati Azerbaijan ilipolivamia jimbo linalozozaniwa la Nagorno-Karabakh mwezi uliopita.