1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Putin aitisha Finland baada ya kujiunga na jumuiya ya NATO

18 Desemba 2023

Rais wa Urusi Vladimir Putin ametoa vitisho kwa nchi mwanachama mpya wa jumuiya ya kujihami ya NATO na jirani yake Finland kwa kile alichosema nchi hiyo huenda ikapata "matatizo yasiyojulikana."

https://p.dw.com/p/4aHHJ
Rais wa Urusi Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Alexander Zemlianichenko/REUTERS

Vitisho hivyo amevitoa kwenye mahojiano ya televisheni.

Kwenye mahojiano hayo, Rais Vladimir Putin amesema kwamba awali hakukuwepo na matatizo ila kwa sasa yatakuwepo.

Akionekana kuzungumzia kuhusu uamuzi wa Finland wa kujiunga na jumuiya ya NATO, kiongozi huyo wa Kremlin ameonyesha kutofurahishwa na uamuzi huo.

Finland iliamua kuomba uanachama wa NATO baada ya Urusi kuivamia Ukraine mnamo Februari mwaka jana.

Sweden ambayo ni jirani ya Finland, nayo pia imetuma ombi la kujiunga na NATO japo haijapata uungwaji mkono kamili kutoka nchi wanachama 31 wa jumuiya hiyo ya kujihami, hasa kutokana na upinzani kutoka Uturuki.