1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Puigdemont atangaza kurudi Catalonia

8 Agosti 2024

Kiongozi wa Wakatalani wanaotaka kujitenga, Carles Puigdemont, ametangaza azma ya kurejea nchini kwake katika siku ambayo bunge la Catalonia linatazamiwa kumchaguwa kiongozi mpya.

https://p.dw.com/p/4jDot
Carles Puigdemont
Carles PuigdemontPicha: Adria Puig/Anadolu/picture alliance

Puigdemont, ambaye anaweza kukamatwa na mamlaka za Uhispania, ameandika kwenye ukurasa wa X kwamba yuko tayari kurejea. Chama chake, JxCAT, kimetangaza mapokezi rasmi ya kiongozi wao majira ya saa 3:00 asubuhi nje ya bunge la Catalonia, mjini Barcelona.

Kuwasili kwa Puigdemont kunakhofiwa kuvuruga sherehe za kuapishwa Salvador Illa, wa chama cha Kisoshalisti, kuwa kiongozi mpya wa Catalonia.

Soma zaidi:Kiongozi wa zamani wa Catalonia atoa sharti la kuinusuru serikali ya Uhispania 

Illa, anatazamwa kama mshirika mkubwa wa Waziri Mkuu wa Uhispania, Pedro Sanchez.  

Chama chake kilipata viti vingi bungeni ingawa havikutosha peke yake kuunda serikali, huku chama cha Puigdemont kikiwa cha pili.