1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PRAGUE. Waziri mkuu wa jamhuri ya Ucheki ajiuzulu.

25 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFJR

Waziri mkuu wa jamhuri ya Ucheki, Stanislav Gross, amejiuzulu. Kuijiuzulu kwake ni sehemu ya makubaliano yaliyoafikiwa juma lililopita, yatakayoshuhudia waziri wa maendeleo ya mikoa, Jiri Paroubek, akichukua wadhifa huo wa waziri mkuu.

Gross alilazimika kuondoka madarakani kufuatia hatua ya chama kimoja katika serikali yake ya mseto kujiondoa serikalini kwa sababu ya kashfa inayohusiana na matumizi ya fedha kununua ghorofa ya kifahari mjini Prague. Gross amekanusha kuhusika katika kashfa hiyo.