1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Postecoglou: Kandanda lastahili kuleta watu pamoja

23 Oktoba 2023

Nchini England usiku wa Jumatatu kutachezwa mechi moja ya ligi ambapo Tottenham Hotspur ambao wameuanza msimu vyema chini ya Ange Postecoglou wataingia uwanjani kuwakaribisha Fulham.

https://p.dw.com/p/4XuOq
Ligi ya Mabingwa Ulaya | RB Leipzig vs. Celtic Glasgow
Kocha wa Tottenham Hotspur Ange PostecoglouPicha: Ronny Hartmann/AFP/Getty Images

Spurs watakwea hadi kileleni mwa ligi hiyo iwapo watapata ushindi usiku wa leo.

Kuelekea mechi hiyo kocha wa Spurs Postecoglou ametoa wito wa amani ukizingatia kwamba wachezaji katika ligi hiyo wamekuwa wakitoa heshima zao kwa walioaga dunia katika mapigano yanayoendelea huko Mashariki ya Kati katika vita vya Israel dhidi ya kundi la Hamas.

"Nafikiri dhima kuu ya vilabu vya kandanda katika wakati kama huu ni kutoa mchango ambao vimekuwa vikitoa. Sehemu ambayo watu wanaweza kutorokea na kuungana pamoja kushabikia klabu yao ya kandanda na labda iwaondoe kutoka kwenye matatizo waliy nayo. Nafikiri hiyo ndiyo dhima kuu ya klabu yoyote ya kandanda," alisema Postecoglou.

Chanzo: AFPE/Reuters