1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Aliyewapiga risasi wanafunzi wa Kipalestina Marekani asakwa

27 Novemba 2023

Polisi nchini Marekani inaendesha msako wa kumtafuta mtu mmoja mwenye bunduki aliyewapiga risasi na kuwajeruhi wanafunzi 3 wa chuo kikuu wenye asili ya Kipalestina huko katika jimbo la Vermont jana jumapili.

https://p.dw.com/p/4ZTHu
Marekani | Polisi
Moja ya gari za polisi nchini Marekani Picha: Chris Delmas/AFP/Getty Images

Taarifa ya polisi imesema mwanaume mwenye bunduki ndogo aliwapiga risasi wanafunzi hao jirani na Chuo Kikuu cha Vermont na kisha kutokomea kusikojulikana. 

Polisi imesema wote watatu wanapatiwa matibabu hospitali huku wawili kati yao wakionesha kupata ahueni lakini mmoja bado yuko kwenye hali dhaifu kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata.

Inaarifiwa watatu hao walikuwa wakizungumza kwa lugha ya kiarabu pale waliposhambuliwa na waendesha mashtaka wanashuku kuwa kisa hicho huenda kimechochewa na chuki.

Shambulizi hilo limetokea katika wakati visa vya chuki dhidi ya waislamu na wayahudi vimeongezeka nchini Marekani tangu kuzuka kwa mapigano kati ya Israel na kundi la Hamas huko Ukanda wa Gaza.