1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi ya Kenya na Haiti kuyafurusha magenge

29 Agosti 2024

Vikosi vya Haiti kwa kushirikiana na polisi wa Kenya waliotumwa nchini humo, wameanzisha operesheni ya pamoja ya kuyafurusha magenge ya wahalifu.

https://p.dw.com/p/4k2St
Haiti Port-au-Prince | Polizisten aus Kenia | Hilfe zur Bekämpfung von Bandengewalt
Picha: Marckinson Pierre/dpa/AP/picture alliance

Vikosi hivyo vinatakakuyaondoa magenge hayo kutoka mojawapo ya vitongoji hatari vya mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince.

Hayo yameelezwa jana usiku na Waziri Mkuu wa Haiti Garry Conille alipokuwa katika hospitali mjini humo ambapo watu watatu walikuwa wakipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa katika operesheni hiyo katika kitongoji cha watu masikini huko Bel Air.

Kiongozi huyo amesema amechoshwa na kwenda kila mara kwenye mazishi ya maafisa wa polisi na kwamba ni lazima washughulikie ipasavyo tatizo ya ukosefu wa usalama. Zaidi ya mauaji 3,200 yameripotiwa nchini Haiti kuanzia Januari hadi

Mei mwaka huu.