1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Macron aagiza usalama kuimarishwa Ufaransa

14 Oktoba 2023

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, leo ameagiza kuongezwa kwa wanajeshi 7,000 ili kuimarisha usalama, siku moja baada ya mwalimu mmoja kushambuliwa kwa kisu na kuuwawa karibu na shule, kaskazini mwa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4XXAv
Frankreich Fernsehansprache von Präsident Macron zu Israel und Gaza
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron Picha: Eliot Blondet/abaca/picture alliance

Tukio hilo linalohusishwa na itikadi kali za kiislamu lilitokea baada ya kijana wa miaka 20 kumchoma kisu mwalimu huyo na kuwajeruhi vibaya watu wengine wawili kwenye mji wa Arras. Kufikia sasa watu kumi wamekamtwa.

Soma pia: Polisi Ufaransa wafanya misako baada ya mwalimu kuchinjwa

Kulingana na ofisi ya Macron, wanajeshi hao wa kuimarisha usalama watasambazwa kuanzia Jumatatu, kama sehemu ya operesheni inayoendelea ambayo hulinda doria katikati mwa miji mikubwa na maeneo ya utalii.

Tahadhari za kiusalama zinaendelea pia kuchukuliwa wakati nchi hiyo ikiwa ni mwenyeji wa kombe la dunia wa mchezo wa Raga.

Ufaransa imekuwa ikilengwa na mfululizo wa mashambulizi yanayohusishwa na itikadi kali za kiislamu kwa miaka mingi. Moja ya matukio mabaya zaidi lilikuwa Novemba 2015 ambapo watu wenye silaha na washambuliaji wa kujitoa muhanga kwa wakati mmoja walishambulia kumbi za starehe na migawaha mjini Paris.