1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi wa Kenya wafyatua mabomu ya machozi kwa waandamanaji

25 Juni 2024

Maafisa wa polisi wameshika doria katika maeneo mbalimbali ya mji mkuu wa Kenya, Nairobi wakati wa maandamano ya kupinga mswada tata wa fedha. Inaripotiwa kuwa maduka na biashara nyingi zimefungwa mjini humo.

https://p.dw.com/p/4hT34
Nairobi, Kenya
Maandamano ya kupinga mswada tata wa fedha yafanyika katika sehemu nyingi nchini Kenya Picha: Monicah Mwangi/REUTERS

Tukio hilo linatokea wakati huu ambapo duru zinaeleza kunafanyika maandamano ya taifa zima kupinga mswada wa nyongeza ya kodi.

Kumeripotiwa msururu mkubwa wa polisi katika jiji la kibiashara la Nairobi huku maafisa wa polisi waliovalia mavazi ya kutuliza ghasia wakiwazuia watu kuingia bungeni, ambapo wabunge wanajadili mswada tata wa fedha wenye mapendekezo ya kodi.

Rais wa Kenya asema yuko tayari kuzungumza na Gen-Z

Kwingineko, umati wa watu ulikuwa ukiandamana katika mji wa bandari wa Mombasa, katika ngome ya upinzani ya Kisumu, na ngome ya Ruto huko Eldoret.

Maandamano hayo ambayo hasa yanaongozwa na vijana maarufu kama Gen-Z yalioanza juma lililopia, yameicha bumbuwazi serikali ya Rais William Ruto, huku kiongozi huyo wa Kenya akisema mwishoni mwa juma kwamba yuko tayari kuzungumza na waandamanaji.

Mmoja auwawa, 200 wajeruhiwa katika maandamano ya Kenya