1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi wa Kenya waendelea kuwasili Haiti kuyadhibiti magenge

4 Julai 2024

Viongozi wa Haiti wanakabiliwa na changamoto kubwa katika wakati vikosi vya polisi Kenya vinawasili katika nchi hiyo inayokumbwa na ghasia.

https://p.dw.com/p/4hrjy
Haiti Port-Au-Prince | Garry Conille |
Waziri Mkuu wa Haiti Garry Conille anasema polisi ya Kenya itasaidia kuyadhibiti magende ya uhalifuPicha: Ralph Tedy Erol/REUTERS

Serikali ya mpito ya Haiti na waungaji mkono wake wa kimataifa wanasema ujumbe wa polisi wa Kenya ni muhimukatika kurejesha udhibiti kutoka kwa magenge ambayo yameteka sehemu kubwa ya mji mkuu, Port Au Prince. Magenge hayo yamekuwa pia yakifanya matendo ya kifedhuli ya wizi na mauaji.

Ghasia zilizoikumbuka nchi hiyo zilisababisha serikali ya waziri mkuu Ariel Herny kujiuzulu. Hata hivyo sasa hivi kuna nafasi mpya ya matumaini imepatikana. Ujumbe wa kimataifa wa kusaidia kurejesha utulivu umeanza kuwasili. Ujumbe huo unaongozwa na Kenya iliyoahidi kutuma polisi 1,000 kuisadiia Haiti.

Kikosi cha polisi kinachoelekea Haiti
Kenya iliahidi kutoa polisi 1,000 kujiunga na kikosi cha kimataifa kinachosaidia Haiti kupambana na magengePicha: REBECCA NDUKU/PRESIDENTIAL COMMUNICATION SERVICE/EPA

Tayari kikosi cha polisi 200 kiliwasili Port au Prince siku kadhaa zilizopita. Waziri Mkuu wa mpito wa Haiti Garry Conille tayari amekimwagia sifa kikosi hicho akisema kimewasili na kuanza kazi nzuri marta moja. Pamoja na hayo Conille yuko njiapanda kwa sababu ujumbe wa kusaidia kurejesha amani Haiti haukunza na kikosi cha Kenya. Hivyo inafaa azingatie kwa umakini ukweli huo huku akitafuta uzani pia katika kuwaridhisha watu wa Haiti kwa kuiandaa nchi hiyo kufanya uchaguzi.  Vikosi vilivyotumwa hapo kabla ikiwemo na kutokaMarekani havikufanikiwa kusuluhisha tatizo la magenge ya uhalifu ya Haiti. Hivi sasa tayari kuna hisia kwamba pindi tu polisi wa Kenya watakapo ondoka hali itarejea kuwa kama zamani magenge yakitawala kwa ufedhuli.

 Hayo yanaelezwa waziwazi na baadhi ya wakaazi wa mji mkuu.

"Suluhisho la kweli halitatoka kwa wageni. Sio jukumu lao," amekaririwa mmoja wa wakaazi akisema huku akitoa wito kwa wanasiasa wa nchi hiyo yenye machafuko "kuungana ili kusonga mbele."

Machafuko Haiti
Magenge ya uhalifu yanadhibiti maeneo mengi ya mji mkuu wa Haiti Port-au-PrincePicha: Odelyn Joseph/AP Photo/picture alliance

Majukumu ya serikali hiyo ya mpito mi mengi na makubwa sana kama kurejesha amani na kuondoa mizozo ya kisiasa.Serikali inatarajiwa pia kulinda haki za kibinadamu na kuwawekea raia wake usalama.Pia Conile na wenzake wanatarajiwa kuweka mikakati ya uchaguzi utakao kua wa kwanza tangu 2016

Kulingana na Francois Pierre Louis profesa wa sayansi ya siasa katika chuo cha New York Queens ; Hakuna afisa nchini Haiti ambaye amechaguliwa kikatiba na ni hali isiyoeleweka kwa kuwa kila kitu  nchini Haiti hivi sasa ni kinyume cha katiba, na si halali.

Maswali yameibuka jinsi polisi wa Kenya watakabiliana na magenge nchini Haiti.Hivi majuzi polisi wa Kenya wameshutumiwa kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji mjini Nairobi.Polisi wamedhaniwa kuwauwa zaidi ya watu 30 kwa mujibu wa mashirika ya kibinadamu

Ni kwa nini Kenya imejitokeza kupeleka polisi wake Haiti?

Ingawa viongozi wa sasa wa Haiti  hawakuchaguliwa, ukosefu wa udhibiti wa serikali unamaanisha kuwa kupiga kura itakuwa karibu haiwezekani, kwa mujibu wa wataalamu.Baada ya tetemeko la ardhi kuiharibu nchi hiyo mwaka 2010, Marekani, miongoni mwa nchi nyingine, zilishinikiza uchaguzi, uliocheleweshwa na maafa hayo, ufanyike haraka iwezekanavyo.

Matokeo yake yalikuwa kura iliyosimamiwa vibaya, iliyokumbwa na ghasia iliyokataliwa na wengi wakiitaja kuwa haramu.

Zaidi ya hitaji la haraka la kurejesha usalama kuna matatizo makubwa zaidi ya kurejesha uaminifu -- ikiwa ni pamoja na suala la uhusiano kati ya wanasiasa wa Haiti na magenge.

Mwandishi: Daniel Muteti