1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Polisi wa Italia wakamata shehena kubwa ya Dawa ya Kulevya

16 Mei 2023

Polisi kusini mwa Italia wamekamata takriban kilo 2,700 za dawa za kulevya aina ya Kokeini iliyokuwa imefichwa kwenye kontena mbili za jokofu zilizokuwa na bidhaa ya ndizi na ambazo zilisafirishwa kutoka nchini Ecuador.

https://p.dw.com/p/4RPFj
Ecuador | Drogen
Picha: Dolores Ochoa/AP Photo/picture alliance

Polisi wanaoshughulikia ulanguzi wamesema dawa hizo za kulevya zenye thamani ya zaidi ya dola milioni 880 na ambazo zilikuwa zinapelekwa Armenia, zimekamatwa kwenye bandari ya Gioia Tauro kusini magharibi mwa Italia.

Siku chache zilizopita, polisi walifanikiwa kukamata katika bandari hiyo kilo 600 ya kokeini kwenye makontena ya matunda kutoka Ecuador. Shehena hizi zilikuwa zinaelekea katika mataifa ya Italia, Croatia, Ugiriki na Georgia.

Eneo la Calabria inakopatikana bandari hiyo linafahamika kuwa ngome ya magenge makubwa zaidi ya uhalifu kama "Ndrangheta" ambayo yanahusika na biashara haramu ya dawa za kulevya.