1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Uhuru wa vyombo vya habari

Polisi Vietnam yamkamata mwandishi wa habari mashuhuri

8 Juni 2024

Polisi nchini Vietnam imemkamata mwandishi wa habari mashuhuri wa kujitegemea Huy Duc kwa madai ya kutumia vibaya uhuru wa kidemokrasia, kuidhoofisha serikali katika makala yake aliyoichapisha Facebook.

https://p.dw.com/p/4gom1
Rais mpya wa Vietnam To Ham
Rais mpya wa Vietnam To HamPicha: Pham Trung Kien/VNA via AP/picture alliance

Polisi nchini Vietnam imemkamata mwandishi wa habari mashuhuri wa kujitegemea Huy Duc kwa madai ya kutumia vibaya uhuru wa kidemokrasia, kuidhoofisha serikali katika makala yake aliyoichapisha katika mtandao wa Facebook.

Kulingana na wizara ya usalama wa umma, mwandishi huyo mwenye umri wa miaka 62 alikamatwa kwa uchunguzi wa chapisho linalotajwa "kukiuka haki, maslahi ya serikali, ya watu binafsi na hata mashirika".

Mwandishi Huy Duc ni luteni wa zamani mwandamizi na amewahi kufanya kazi katika magezeti kadhaa makubwa nchini Vietnam kabla ya kufutwa kazi mnamo mwaka 2009.

Chama cha Kikomunisti cha Vietnam kimekuwa na hatua kali dhidi ya waandishi wa habari. Shirika la waandishi wa habari wasio na mipaka RSF, limeiorodhesha nchi hiyo katika nafasi ya 174 kati ya nchi 180 katika masuala ya uhuru wa vyombo vya habari.