1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi Ujerumani yaanzisha msako wa wapinga serikali

23 Novemba 2023

Maafisa wa polisi kiasi 280 wameendesha msako katika majumba kadhaa katika majimbo manane ya Ujerumani katika hatua inayohusiana na uchunguzi wa kundi la wajerumani wasioutambuwa mfumo wa sasa wa serikali.

https://p.dw.com/p/4ZN0m
Deutschland, Berlin | Razzia im Zusammenhang mit dem Verbot der Hamas und von Samidoun
Polisi wa Ujerumani wakiwa katika msako mjini BerlinPicha: Fabrizio Bensch/REUTERS

Wafuawasi hao pia mihimili ya dola bunge na mahakama. Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na shirika la habari la kijerumani, dpa washukiwa wanadhaniwa kuunda kundi la kihalifu. Katika miezi ya hivi karibuni, polisi wa Ujerumani wameendesha msako mara kadhaa dhidi ya makaazi na ofisi za watu wanaoshukiwa kuwa wanachama  wa vuguvugu hilo.Mnamo mwezi Oktoba polisi katika majimbo mengi ya Ujerumani walifanya upekuzi kwenye makaazi yawanaoshukiwa kuwa wanachama waliohusishwa na kundi linalojita Mshikamano wa Wazalendo, United Patriots, ambalo linatajwa lilihusika kuandaa mapinduzi na katiba mpya chini ya msingi wa utawala wa Ujerumani wa mwaka 1871.Watu watano walishtakiwa kwa kupanga mapinduzi na kudhamiria kumuua waziri wa afya wa shirikisho Karl Lauterbach.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW