1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Zaidi ya watu 700 wakamatwa nchini Ufaransa

2 Julai 2023

Zaidi ya watu 700 wamekamatwa na polisi nchini Ufaransa Jumamosi usiku wakati wa ghasia za kupinga ukatili wa polisi kutokana na kifo cha kijana Nahel aliyekuwa na miaka 17

https://p.dw.com/p/4TJpH
Frankreich Unruhen in Frankreich - Paris
Picha: Nacho Doce/REUTERS

Wizara ya mambo ya ndani nchini humo imesema katika vurumai hiyo polisi 45 walijeruhiwa. Machafuko yaliibuka nchini humo kutokana na kifo cha kijana Nahel aliyekuwa na miaka 17, aliyeuwawa wakati akiendesha gari kwa kupigwa risasi na polisi wakati wa ukaguzi wa barabarani.

Waandamanaji waharibu mali

Waandamanaji wanaopinga mauaji hayo wengi wao wakiwa ni vijana wadogo wamechoma magari na kuharibu mali pamoja na miundombinu. Polisi anayetuhumiwa kwa mauaji ya kijana huyo amekamatwa na anakabiliwa na mashtaka ya kuua bila kukusudia.