1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi nchini Morocco wamewakamata watuhumiwa watatu zaidi

Sekione Kitojo
20 Desemba 2018

Watuhumiwa watatu zaidi katika mauaji ya watalii wawili wanawake kutoka Norway na Denmark, wamekamatwa.

https://p.dw.com/p/3AQm4
Marokko zwei Touristinnen wurden im Dorf Imlil tot aufgefunden
Picha: Getty Images/AFP/KECH24 Moroccan News Channel

Polisi  nchini  Morocco  wamewakamata  watuhumiwa watatu  zaidi  katika  mauaji  ya  watalii  wawili  wanawake , kutoka  Norway  na  Denmark, katika  milima  ya  Atlas.

Siku  moja  kabla  maafisa  nchini  Morocco walisema wanawatafuta  watuhumiwa  wengine  watatu  baada  ya mtu  mmoja  kukamatwa  mjini  Marrakech. Mwendesha mashitaka  mkuu  wa  serikali  amesema  mtu  huyo ambaye  yuko  kizuwizini  ni mwanachama  wa  kundi  la wanmgambo, lakini  hakutoa  jina  la  kundi  hilo.

Miili  ya  Louisa Vesterager Jespersen mwenye  umri  wa miaka  24, kutoka  Denmark   na  Maren Ueland , mwenye umri  wa  miaka  28 kutoka  Norway , ilipatikana  siku  ya jumatatu   katika  eneo  la  mbali  karibu  na  Imlil, katika njia  kuelekea  Toubkal,  kilele  cha  juu  kabisa  cha milima  katika  taifa  hilo  la  Afrika  kaskazini  na  eneo maarufu  kwa  watalii.