1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBrazil

Aliyepanga jaribio la kumuua Rais wa Brazil akamatwa.

5 Agosti 2023

Polisi nchini Brazil wamemkamata mtu mmoja kwa tuhuma za kupanga jaribio la kumuua Rais Luiz Inacio Lula da Silva kabla ya mkutano wa Amazon utakaofanyika wiki ijayo.

https://p.dw.com/p/4Uo8Z
Lula da Silva bei einer Pressekonferenz mit Maduro, Präsident von Venezuela.
Picha: Frederico Brasil/TheNews2/IMAGO Images

Polisi nchini Brazil wamemkamata mtu mmoja kwa tuhuma za kupanga jaribio la kumuua Rais Luiz Inacio Lula da Silva kabla ya mkutano wa Amazon utakaofanyika wiki ijayo. Lula anatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele juu ya kulinda msitu wa Amazon utakaofanyika kwenye jimbo la Para nchini Brazil. Polisi imesema mtu huyo alikamatwa kwa kutoa kauli kwamba anapanga kumpiga risasi Rais Lula na kuongeza kuwa polisi walifanya msako kumsaka mtu mwingine anayetuhumiwa kutoa vitisho mtandaoni dhidi ya kiongozi huyo wa Brazil. Mtuhumiwa wa kwanza alisema alipanga kumpiga risasi rais Lula tumboni. Mtu huyo alikamatwa baada ya raia mmoja kupiga ripoti kwa polisi.