1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPoland

Poland yaishtumu Ujerumani kwa kuingilia mambo yake ya ndani

25 Septemba 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Poland Zbigniew Rau ameishutumu Ujerumani kwa kuingilia masuala yake ya ndani kwa kuitaka kutoa ufafanuzi kuhusu tuhuma za kashfa ya rushwa katika utoaji visa kwa raia wa Afrika na Asia.

https://p.dw.com/p/4WlXM
Waziri wa mambo ya nje wa Poland Zbigniew Rau wakati wa mkutano wake na mwenzake wa Ujerumani Annalena Baerbock mnamo Mei 24, 2022
Waziri wa mambo ya nje wa Poland Zbigniew RauPicha: Tobias Schwarz/AFP/dpa/picture alliance

Rau ametoa wito kwa  kansela wa Ujerumani Olaf Scholz kuheshimu uhuru wa Poland na kumtaka ajiepushe na kauli zinazoharibu mahusiano baina ya mataifa hayo mawili.

Chama tawala chakabiliwa na shinikizo kuhusu madai ya kashfa

Chama tawala cha mrengo wa kulia nchini Poland, kinachojinadi kuwa cha "Sheria na Haki", kinakabiliwa na shinikizo kubwa kuhusu madai ya kashfa hizo kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 15 ambapo chama hicho kinawania pia muhula wa tatu madarakani.

Soma pia:EU, Ujerumani zaitaka Poland kujieleza kuhusu rushwa ya visa

Wiki iliyopita, vyombo vya habari vya Poland viliripoti kuwepo kwa mfumo wa rushwa unaoendeshwa na balozi za Poland kwa watu kutoka barani Afrika na Mashariki ya Kati wanaohitaji kuingia katika eneo la mipaka huru linajumuisha mataifa 26 ya Ulaya.

--