1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPoland

Poland yadokeza kutuma vifaru chapa Leopard 2 Ukraine

19 Januari 2023

Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki amedokeza kwamba nchi yake huenda ikaitumia Ukraine vifaru chapa Leopard 2 kama sehemu ya muungano mpana hata bila idhini ya Ujerumani.

https://p.dw.com/p/4MRdl
Belgien I Mateusz Morawiecki in Brüssel I EU
Picha: Nicolas Landemard/Le Pictorium/MAXPPP/picture alliance

Kauli hii ya Morawiecki inaiongezea Ujerumani shinikizo kuelekea mkutano wa kesho katika kambi ya kijeshi ya Ramstein utakaojadili usaidizi zaidi wa kijeshi kwa Ukraine. Waziri huyo mkuu ameyasema haya alipokuwa akizungumza na televisheni moja ya kibinafsi nchini Poland ambapo amedai kwamba idhini kwa sasa si jambo muhimu na mambo ni mawili, ama wapate idhini hiyo kwa haraka au wafanye kinachohitajika wenyewe.

Poland na washirika wake zimekuwa zikishinikiza kupata idhini ya Ujerumani

Poland na marafiki zake wengine katika Jumuiya ya Kujihami ya NATO wamekuwa wakiishinikiza Ujerumani kuwapa idhini ya kutuma vifaru hivyo vinavyotengenezwa Ujerumani. Haya yanafanyika wakati ambapo Ukraine imetoa wito wa msaada zaidi wa kijeshi ambao inasema utasaidia kuugeuza mwelekeo wa vita hivyo vilivyoanzishwa na Urusi.