1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Poland na Hungary zina tatizo la demokrasia

5 Julai 2023

Kamisheni ya Umoja wa Ulaya imeyanyooshea kidole mataifa ya Poland na Hungary kwa mapungufu yake ya kidemokrasia ambayo yanachochewa na hatua zinazochukuliwa au kutoshughuliwa na serikali za sasa za mataifa hayo.

https://p.dw.com/p/4TSh0
EU Vera Jourová und Didier Reynders PK zum "Rule of Law report 2023" in Brüssel
Picha: Lukasz Kobus/EU

Pamoja na kwamba ripoti ya kila mwaka ya umoja huo kuhusu utawala wa sheria imetaja kuwepo na kiwango fulani cha maboresho kwa mataifa hayo mawili, lakini pia imeyaweka bayana mapungufu mengi yaliyosalia ambayo yanaangazia msuguano kati ya ofisi ya Umoja wa Ulaya yenye makao yake makuu mjini Brussels na mataifa hayo mawili ya Ulaya Mashariki.

Ripoti hii mpya ya kurasa 35 inaliweka wazi moja kati ya matatizo ya kimsingi katika muungano huo wenye mataifa 27, ambao kwa siku zote umekuwa katika jitihada ya kuwa kinara wa demokrasia katika ulimwengu ambao siasa za kiimla zinapata nguvu.

Poland imeendelea kukosa ufadhili wa Umoja wa Ulaya.

Belgien EU-Gipfel in Brüssel
Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban Picha: Nicolas Economou/NurPhoto/IMAGO

Katika ripoti hiyo mpya Poland imetajwa mara kadha na hasa katika  masuala ya kisheria ambayo hayajashughulikiwa kikamilifu licha ya kudumu kwa miaka kadhaa ya mzozo kati ya Umoja wa Ulaya na taifa hilo, na pia kuwepo kwa uamuzi wa Umoja wa Ulaya kuikaitalia Poland kuweza kupata kiasi fulani cha fedha zake za ufadhili.

Ripoti hiyo inaeleza bado kuna "mashaka makubwa" yenye kuhusiana na taasisi ya serikali iliyokusudiwa kulinda uhuru wa mahakama na majaji, na kusema "kuna wasiwasi usio na mashaka uhuru wake."

Mashaka ya uhuru wa mahakama.

Vilevile inasema mashaka makubwa yanasalia katika teuzi za majaji wa mahakama kuu. Ripoti kadhalika imeonesha malalamiko yake kwa serikali ya Warsaw kutokana na uchunguzi wa majaji unaondelea mabao umesababishwa na hukumu zao za kimahakama. Imegusia pia mabadiliko ya sheria ya hivi karibuni ambayo yanawethiri uwezekano wa watu binafisa kugombea katika kuwania nafasi za uongozi wa umma.

Ripoti iliyafanyia tathimini mapendekezo yake ya ripoti kama hii kwa mwaka uliopita na kubaini kuwa mambo kadhaa kuanzia katika suala la uhuru wa mahakama hadi vyombo vya habari na hatua za kupambana na rushwa hakuna hatua zilizopigwa.

Ripoti hiyo imeonekana kutokuwa na makali sana kwa Hungary yenyewe, ambayo imesema  baadhi marekebisho ya sheria yalikuwa yameridhiwa na baadhi ya ukaguzi wa kimahakama na kutkelwzwa kwa uzani stahili.

Soma zaidi:Poland yaimarisha ulinzi wa mpaka na Belarus baada ya kuwasili mkuu wa Wagner

Kwa ujumla ripoti hii ya nne ya mwaka ya Umoja wa Ulaya kuhusu utawala wa sheria katika mataifa wanachama 27 ya umoja huo inabainsha maendeleo kuhusu takriban theluthi mbili ya mapendekezo yake lakini inasema kuwa kumesalia uwepo wa mashaka ya kimfumo katika utawala wa sheria kwa baadhi ya nchi wanachama.

Chanzo: RTR